Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya
Kutofungamana na Siasa ya Upande wowote unaomalizika leo mjini
Teheran, nchini Iran. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine
alisisitiza msimamo wa Tanzania kuendelea kupigania haki, kutetea
wanyonge, kupinga ubeberu na ukandamizaji kote duniani, pia aliiasa
Jumuiya ya Kimataifa kutatua migogoro yote kwa njia ya amani. Mkutano
huo unamalizika leo na Makamu wa Rais, anatarajia kurejea nchini kesho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano mkuu wa 16 wa kimataifa wa
wakuu wa nchi na serikali usiofungamana na upande wowote Duniani,
mkutano huo umeanza leo mjini Teheran Iran.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Abad
Mobin, wakati Makamu wa Rais alipohudhuria mkutano mkuu wa 16 wa
kimataifa wa wakuu wa nchi na serikali usiofungamana na upande wowote
Duniani. mkutano huo umefunguliwa leo mjini Teheran Iran.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)