Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati
alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo
Agosti 12, 2012 kuhudhuria fainali za mashindano ya kimataifa ya Qur-an
yaliyoshirikisha nchi 13, ambapo mshindi alikuwa ni Abdulrahman Salis
Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyeshinda kwa jumla ya Pointi 96.12.
Mmoja
kati ya washiriki wanne walioiwakilisha Tanzania, katika fainali za
mashindano ya kimataifa ya Qur-an, yaliyoshirikisha nchi 13, Omar
Abdallah, akisoma Qur-an wakati akishiriki katika fainali za mashindano
hayo ya Kimataifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini
Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati alipohudhuria na kuwa mgeni rasmi katika
fainali za mashindano ya Qur-an ya kimataifa, yaliyofanyika kwenye
Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi ya Dola za Kimarekani 1250, mshindi wa tatu katika
fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, Ijaaz Mukaddam (22),
kutoka Afrika ya Kusini, aliyepata jumla ya Pointi 95.08 baada ya
kutangazwa washindi wa fainali hizo. Mshindi wa kwanza alikuwa ni
Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyepata Pointi 96.12, wa
pili ni Twalha Ally Mohammed (18) kutoka Philippines, aliyepata Pointi
96.03.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi funguo ya Pikipiki, mshindi wa kwanza kwa watanzania,
Mohammed Omar Mkilalu, baada ya kutangazwa washindi wa fainali za
mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, zilizofanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na mshiriki mdogo kuliko wote katika mashindano hayo ya
Qur-an, ya kimataifa, Suleyman Ahmad (9) kutoka China, aliyeshiriki
katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo
Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Cheti Ustaadh Muhammad Abdullah Balarabe, aliyeongozana na
mshiriki mshindi wa kwanza katika fainali za mashindano hayo ya
Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo
Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Dini ya Kiislamu na washindi
wa tatu Bora wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an,
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya
pamoja na Majaji wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an,
yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)