Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi ya mradi wa skuli ya Istiqama uliopo
katika kijiji cha Mbuyuni Mkoani Pemba Ustadhi Mohd Omar Makame
akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi huo
Mjumbe wa Kamai Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi akikabidhi mchango wa shilingi 800,000/- kusaidia ununuzi wa saruji
kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Tawi la CCM la Makombeni Mkoani
Kisiwani Pemba. Sambamba na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi pia
akakabidhi mchango wa shilingi 300,000/- kwa ajili yha mIlango ya Tawi
hilo.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Tawi la CCM, Makombeni
wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif Ali Iddi aliyetembelea Tawi hilo
kuangalia hatua iliyofikia ya ujenzi wa Tawi hilo.
--
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea
mradi huo.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono miradi yote inayoanzishwa na
Taasisi, Mashirika, Jumuiya na hata Wananchi katika lengo la kustawisha
Maendeleo ya Jamii hapa Nchini.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo
wakati alipokuwa akikagua mradi mkubwa wa ujenzi wa Skuli inayojengwa
na kusimamiwa na Jumuiya ya Istiqama Tanzania hapo katika Kijiji cha
mbuyuni Mkoani Kisiwani Pemba.
Balozi Seif aliuambia uongozi wa wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa
mradi huo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kwamba
miundo mbinu muhimu ya maji, umeme na bara bara inawekwa ili kuona lile
lengo lililokusudiwa la kuanzishwa kwa mradi huo muhimu kwa jamii
linafikiwa.
Aliuagiza Uongozi huo kumuandikia barua mara moja ya changamoto
wanazopambana nzo ambazo zimo ndani ya uwezo wa Serikali Kuu ili iwe
rahisikwake kuziagiza Taasisi husika kupanga mikakati ya kutekeleza
miundo mbinu hiyo.
Balozi Seif alisema atatumia uwezo na nafasi aliyonayo kushawishi
wahisani zikiwemo ofisi za Kibalozi kusaidia ujenzi huo uliolenga kwenda
hadi ghorofa tatu ambao tayari hivi sasa umeshatumia karibu
shilingiMilioni mia tatu { 300,000,000/- }.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Jumuiya hiyo ya Istiqama
Tanzania kwa hatua yake ya kujenga mradi huo mkubwa ambao utasaidia
kusukuma mbele Maendeleo ya Elimu ya Dini na Dunia.
Alisema Jumuiya hiyo inafaa kuungwa mkono na jamii yote Nchini kwa vile
tayari imeshajipanga vyema kuweka mkazo zaidi katika suala la Elimu kwa
kukiandalia mazingira bora kizazi cha sasa.
“ Nimevutiwa sana na mradi huu wa Elimu wenye kuleta faraja
si kwa wakaazi wanaouzunguuka hapa lakini kwa Wananchi wote
Nchini. Naimani kwamba utakapokamilika bila shaka utachukuwa wananfunzi
wa sehemu mbali mbali Nchini”.
Alionyesha furaha yake Balozi Seif.
Mapema Mwenyekiti wa
Kamati ya Ujenzi wa Mradi huo Ustaadhi Mohammed Omar Makame alimueleza
Balozi changamoto wanazopambana nazo wakati huu wa ujenzi.
Ustaadh Mohd Omar alizitaja changamoto hizo kubwa kuwa ni pamoja na
ukosefu a huduma ya maji safi, umeme pamoja na Bara bara licha ya juhudi
walizochukuwa za kuchimba kisima bila ya mafanikio.
Alisema ujenzi wa Skuli hiyo ulioanza tarehe 1/12/2010 utakapokamilika
utakuwa na uwezo wa kuchukuwa wanafunzi 1575, Madarasa 45 , mabweni,
nyumba za walimu pamoja na msikiti lengo likiwa kunyanyua elimu ya dini
sambamba na kuibua vipaji vya wanafunzi.
Mapema asubuhi Balozi Seif akiwa pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alipata fursa ya kutembelea Tawi Jipya
la CCM la Makombeni pamoja na kukagua uhai wa Chama hapo katika mtaa wa
Mweneza.
Akizungumza na Viongozi na Wanachama hao Balozi Seif aliwatahadharisha
katika kipindi hichi cha chaguzi zinazoendelea za chama hicho
wahakikishe wanawachaguwa Viongozi safi watakaokuwa mahiri katika
kutekeleza Sera za chama hicho.
Alisema wakati umefika kwa Wanachama wa chama hicho kuwakataa
wanachama wasiokuwa na msimamo kwa kufikiria kujinufaisha binafsi pamoja
na kuvuruga chama kwa makusudi.
“ Wale
wanaohisi kwamba sera za Chama cha Mapinduzi zimepitwa na wakati kwa
hiyari yao wangeliamua mapema kwenda kwenye vyama vyenye Sera za Dot Com
na kuiachia CCM Yetu inayoamini sera za Serikali mbili Ncchini
Tanzania”. Alifafanua Balozi Seif.
Katika kuunga mkono harakati za kukamilisha ujenzi wa Tawi la CCM
Makombeni
Balozi Seif alichangia shilingi laki nane { 800,000/- } kusaidia ununuzi
wa saruji na kuahidi shilingi 500,000/- za fundi pamoja na Seti ya TV
na DVD yake wakati Mkewe alichangia shilngi laki 300,000/- kusaidia
milango ya Tawi hilo.
Akitoa Taarifa fupi ya ujenzi huo pamoja na uhai wa Chama Katibu wa CCM
WA Tawi la Makombeni Bibi Wahida Mbaraka Mohd alisema ujenzi wa Tawi
hilo umekuja ili kwenda sambamba na hadhi ya chama chenyewe kilivyo.
Bibi Wahida alisema hadi sasa ujenzi huo uliolenga kufikia gharama ya
shilingi milioni 13,920,000/- umeshafikia shilingi milioni 8,000,000/-.
Katibu wa Tawi hilo alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Wanachama wa CCM
wa Tawi hilo wataendelea kuunga mkono sera za Chama chao za kuamini
mfumo wa Serikali mbili Nchini Tanzania.
Alisema Wanachama hao wamejiimarisha kutoghilibiwa na vurumai
zinazojichomoza Nchini za baadhi ya watu kushawishi wananchi juu
yamchakato wa utoaji wa maoni ya Katiba unaolenga kuvunja Muungano.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)