Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiitikia
dua wakati alipofika nyumbani kwa Mzee Ali Haji Pandu huko Mpendae kwa
ajili yakumjuilia hali.) Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza waRais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad leo
alifanya ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa mbali mbali katika
manispaa ya mji wa Zanzibar.
Miongoni mwa wagonjwa aliowatembelea na kuwafariji ni pamoja na Mzee Ali
Haji Pandu anayeishi eneo la Mpendae na Sheikh Habib Ali Kombo
anayeishi Kiembesamaki.
Katika ziara hiyo , Makamu wa Kwanza wa Rais amewaombea wagonjwa hao
wapone haraka ili waweze kujumuika katika shughuli za ujenzi wa Taifa.
Maalim Seif amekuwa na utaratibu wa kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa
na wafiwa mbali mbali Unguja na Pemba, katika jitihada zake za kuwa
karibu zaidi na wananchi.
Na
Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)