JAJI WARIOBA AJIONEA UTENDAJI KAZI WA SEKRETARIETI YA TUME YA KATIBA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

JAJI WARIOBA AJIONEA UTENDAJI KAZI WA SEKRETARIETI YA TUME YA KATIBA

Afisa wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Joseph Warioba kuhusu utendaji kazi wa kitengo wa Hansard wakati alipofanya ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Tume hiyo, siku ya Ijumaa tarehe 24.Julai.2012. Kushoto ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na aliyekaa ni Afisa wa Sekretarieti Bi. Rose Mangili.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Assaa Rashid akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Joseph Warioba wakati alipotembelea kitengo cha Hansard kujionea shughuli zinazofanywa na Kitengo hicho. Wengine katika picha kutoka kulia Mkuu wa Kitengo hicho, Bi. Hanifa Masaninga na aliyekaa ni Afisa wa Sekretarieti Bi Rose Mangili.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Joseph Warioba wakati alipotembelea kitengo hicho na kujionea utendaji kazi wake, siku ya Ijumaa tarehe 24. Julai.2012. Wengine katika picha ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid, Naibu Katibu Katibu, Casmir Kyuki na watendaji wengine wa Sekretarieti ya Tume hiyo.

Afisa wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Ross Kinemo akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati wa ziara yake ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Tume hiyo aiyoifanya siku ya Ijumaa tarehe 24. Julai. 2012. Wengine katika picha kutoka kulia ni Maafisa wa Sekretarieti Bi. Nenelwa Wankanga na Bw. Joseph Ndunguru.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages