Furaha kila sehemu.
Carnival ikiendelea.
Hata watu wazima walikuwepo ndani ya Carnival huku wakipata mambo ya Mbwa Moto (Hot Dog).
Mh Balozi Kallaghe wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallahe(Kulia)akiwa na Frank kwenye Notting Hill Carnival.
Freddy Macha akipiga Filimbi.
Freddy Macha na Frank Katika Notting Hill Carnival.
Freddy Macha na Wadau wakisherekea Carnival.
Polisi katika pozi.
Ni furaha na shangwe tu kwa kila mtu.
Watu wakumwaga.
---
Salaam,
Urban Pulse Creative na Freddy Macha wanakuletea taswira ya Notting Hill Carnival iliyofanyika jana tarehe 27.8.12. Kihistoria
sherehe hii ilifanywa siku 40 kabla ya Pasaka kipindi kinachoitwa LENT (
“Kwaresima“ )ambapo waumini wa Kikristo hujinyima, husali, hutoa sadaka, huomba
msamaha, huungama makosa , kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kwa kufunga (kama wafanyavyo
Wayahudi na pia Waislamu kabla ya Idd El Fitri). Carnival hushereherekewa
kidesturi mwezi wa pili na watatu (Brazil, Ujerumani, nk) lakini nchi
mbalimbali ( mathalan Uingereza, Japan,
Cape Verde nk) zimegeuza tarehe kufuatana na tamaduni au matakwa yao. London ni Jumapili na
Jumatatu ya mwisho wa mwezi Agosti ambapo hamna kazi (huitwa Bank Holiday).
Carnival ni neno lenye asili ya Kilatini "Carne Vale" –maana yake “Kwaheri” (Vale) “Nyama” (Carne)
Baadhi
ya nchi maarufu kwa Carnival
1.
Brazil
– Rio ni Samba na Bahia ni siku tano za muziki juu ya malori makubwa- Feb na
March
2.
Trinidad
na Tobago- Mwezi Feb na March kabla ya
Pasaka, athiri sana Carnival ya London kwa muziki wake wa Soca na ngoma za
chuma („steel pans“
3.
Nchi
za Kiafrika zenye asilia ya Kireno- husheherekea Carnival, Maputo, Luanda na
visiwa vya Cape Verde- ambapo Carnival inaitwa “Mindelo“....(mji mkuu wa Cape
Verde). Carnival ya Mindelo ni maarufu na kubwa kuliko zote Afrika.
4.
Asakusa,
Japan. Carnival la Japan lenye mahadhi ya Samba na Brazil kila mwaka mwisho wa
mwezi wa Agosti. Vutia watu laki moja.
Muasisi mkuu wa Carnival ya London ni Claudia Jones- mwanamke mwenye asilia ya
Trinidad aliyehamia Uingereza mwaka 1955. Alikuwa mwanahabari aliyepigania haki
za watu weusi. Mwaka 1959 alianzisha Carnival ya kwanza katika kitongoji cha St
Pacrais. Sherehe hii ilivutia sana Habari na ilitangazwa katika BBC. Claudia
Jones alifariki mwaka 1964 kutokana na maradhi ya moyo na kifua kikuu. Amezikwa
kando ya kaburi la Karl Marx, High Gate, London kaskazini.
Asanteni,
Urban Pulse wakishirikiana na Freddy macha
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)