Mchezaji
wa timu ya Yanga, Juma Abdul, akichuana kuwania mpira na beki wa
Atletico, Henry Mbazumutima, wakati wa mchezo wao wa fungua dimba ya
michuano ya kombe la Kagame, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inaandaliwa na Shirikisho la vyama
vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA. Katika mchezo huo Yanga
imeanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 2-0 na Atletico, huku
mabao hayo yakiwekwa kimiani na Olivier Ndikumana katika dakika ya 81 na 90+3.
Wachezaji
wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali
katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.Picha Na Sufiani Mafoto Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)