Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp ambao wapo kwa ajili ya kutoa
huduma katika banda la Benki hiyo katika viwanja vya Maonesho ya
Kimataifa ya Biashara maarufu Saba Saba wakiwa katika picha ya pamoja
mbele ya Banda lao linalotoa huduma kamili za Kibenki.
Afisa
Masoko wa Twiga Bancorp Limited, Adelbert Archerd Tibikunda akiwa
amekamatia tuzo ya Century International Gold Quality ERA waliyo ipata
Genever kwa huduma bora .
Katika
Banda la Twiga Bancorp wateja wanapata fursa ya kuweka fedha zao papo
hapo baada ya kufanya mauzo ndani ya Saba Saba. Yanini utembee na fedha
nyingi wakati Benki ya twiga ipo nawe pale ulipo.
Fedha
katika ATM ni kwa saa 24, siku 7 za wiki, mwezi mzima na siku 360.
Huduma hii katika banda la Twiga hafungwi mwaka mzima.
Utoa huduma bora ndio nguzo na ngao ya Twiga Bancorp, pichani ni mteja akiwa na furaha wakati akizungumza na Afisa
Mwandamizi Mwendeshaji wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Lydia
Matembel, alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonesho Saba Saba.
Ofisa
wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Ernest Kikwasi, akitoa maelezo kwa
wananchi waliotembelea banda hilo jana juu ya akaunti maalum ya watoto.
Twiga Bancorp ni miongoni mwa benki zinazoshiriki katika Maonesho ya 36
ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu JK Nyerere barabara ya Kilwa huku wakitoa huduma kamili za
kibenki.
Mteja
wa Twiga Bancorp akitoka kupata huduma katika banda la Benki hiyo kwa
furaha baada ya kufanikiwa kutimiza alichotaka kwa wakati.
Wateja wakipata huduma ya kubadili fedha katika banda la Twiga Bancorp.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)