Mmoja wa majaji wa shindano
la Serengeti Dance la Fiesta 2012 lililofanyika kwenye Club ya Mawingu
jioni ya leo,jijini Arusha ,Hamis Mandi a.k.a B Dozen kutoka kipindi cha
XXL kinachorushwa na redio ya Clouds FM,akikabidhi kitita cha shilingi
milioni moja kwa kundi shindi la shindano hilo liitwalo Contagious Crew
Mwendesha shindano hilo pichani
kati,Nikson akisoma majina ya makundi mawili yaliyoingia fainali na
hatimae kulipata kundi moja mahiri kabisa na kundi la Contigious Crew
limeibuka mshindi na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja taslim
na kreti moja ya bia ya Serengeti,ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha
la Fiesta 2012.
Pichani majaji wa shindano la Serengeti
Dance la Fiesta 2012 wakijadiliana jambo wakati wa mchuano mkali wa
shindano hilo lililokutanisha makundi manne,ambayo ni Tp Jackson,New
Kings,B-Boy Dance pamoja na kundi la Contigious Crew.Kulia ni Jaji Msami
kutoka THT na shoto ni Mtangazaji kutoka Clouds TV,Issa Kwisa
Sehemu ya washabiki wa Serengeti Dance la Fiesta 2012 wakivutiwa zaidi na shindano hilo lilipokuwa likiendelea ukumbini humo.
Kila kundi lilionesha umahiri wake wa kucheza,huku kwa aliyeonekana kufanya vyema shangwe na miluzi ilitawala kila kona.
Palikuwa hapatoshi jioni ya leo ndani ya
Club ya Mawingu wakati wa shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012
likifanyika,ambapo kila kundi lilionesha umahiri wake wa kuyarudi
mangoma kwa staili ya kipekee kabisa.Pichani mcheza shoo wa kundi la
B-Boy Dance akionesha umahiri wake wa kucheza.
Vijana mbalimbali waliojitokeza kwa
wingi kwenye shindano la Serengeti Dance la Fiesta 2012,ambapo mshindi
alifanikiwa kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja na kreti moja la
bia mshindi wa pili aliibuka na kreti la bia ya serengeti,ambao ndio
wadhamini wakuu wa tamasha hilo kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)