Ofisa
habari wa mabingwa wa soka wa Tanzania, Simba SC, Ezekiel Kamwaga
(kulia) akimkabidhi funguo ya Pikipiki Shabiki wa timu hiyo, Abubakari
Hamis (katikati) kutoka Arusha baada ya kuibuka mshindi katika bahati
nasibu ya Simba Fan Club katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es
Salaam, jana. Kushoto ni Meneja wa kampeni hiyo, Talib Rashid, kutoka
kampuni ya Push Media Moobile. Washiriki wa bahati nasibu hiyo
wanatakiwa kutuma neno Simba kwenda kwenye namba “15678” na kuingia
katika droo.
************************************
Na Mwandishi wetu
KLABU
ya Simba imewataka wapenzi na mashabiki wake kuendelea kujiunga na
huduma ya kutuma ujumbe mfupi kupitia huduma ya Fan Simba Club ili
kupata taarifa mbalimbali za Simba ikiwemo matokeo ya michuano ya kombe
la Kagame inayotarajia kuanza Julai 14 mwaka huu na masuala ya Usajili.
Akizungumza
Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki
kwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Fan Simba, Ofisa Habari wa Klabu hiyo
Ezekiel Kamwaga alisema kupitia huduma hiyo mashabiki wa Simba watapokea
taarifa za kila siku ambazo wao watakuwa wa kwanza kuzipata kupitia
huduma hiyo.
Alisema
pia itaisaidia klabu ya Simba kujiongezea mapato yatakayoiwezesha klabu
hiyo kuendesha mambo yake katika ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na
kusajili wachezaji wazuri.
Kwa
upande wake Meneja Kampeni wa Kampuni ya Push Mobile Talib Rashid
ambao wameingia mkataba na klabu ya Simba kupitia huduma ya sms Fan
Simba Club wamefunga droo ya bahati nasibu waliokuwa wakiichezesha kwa
klabu ya Simba kupitia huduma hiyo kwa kutoa pikipiki na bajaji.
Bahati
nasibu hiyo iliyokuwa ikichezwa kwa kipindi cha miezi mitatu sasa
imefungwa kwa kuwapata washindi ambao ni wanafunzi wa shule za Sekondari
huku mmoja akiwa ni Tito Zakaria kutoka shule ya Sekondari ya Mong'ola
iliyopo Dodoma aliyejishindia pikipiki na Mohamed Ibrahim kutoka shule
ya Sekondari ya Chandama iliyopo Kondoa na kujishindia bajaji.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)