Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa
Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini,
Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar.
Wanafunzi hao wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu
cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa wameongozana na Watendaji Wakuu wa
Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete Ikulu
jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa
ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na
ubalozi wa Tanzania Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu
wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini
Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya
kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na
ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama
hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema
amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama
za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio
ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu
ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)