Wateja wa Benki ya NMB, Victoria
Maliseli, Ramadhan Mguya,Rehema Mohamed,Rose Mandera na Richard Makara
wakifurahia kupata zawadi ya mabati 50 kila mmoja na tani ya saruji
kila mmoja(mabati wawili kushoto na tani ya saruji watatu kulia) pamoja
na Mkuu wa idara yaMasoko na mawasiliano wa NMB Imani Kajula
Mteja wa NMB Bi. Victoria Marisel akipokea mfano
wa hundi yenye thamaniya mabati 50 kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja
wa NMB tawi la NMB Airport, Deogratius Mahawe
Benki ya NMB jana imekabidhi zawadi za tani za saruji na mabati kwa
washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya ‘Jenga maisha yako na NMB’ iliyofanyika terehe 11 Julai
2012.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika katika tawi la NMB
Airport, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula
alisema kwamba, “NMB sasa inawezesha ndoto za watu kuwa kwelileo
tunakabidhi tani za saruji na mabati.Hatimae ndoto za washindi sasa
zimekuwa kweli na tunaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia
ya kujiwekea akiba lakini itasaidia wateja walioshinda kufikia malengo
waliojiwekea na pia kuboresha maisha yao”.
NMB kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka akiba ili kutimiza
malengo mbalimbali waliyojiwekea yakiwa ni kujenga nyumba,kusomesha
watoto na kufikia malengo mengine muhimu maishani mwao,
ilizindua promosheni inayowezesha wateja wa NMB Bonus Account an NMB
Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda tani ya saruji,mabati
ya kuwezeka,amana maradufu,ada za shule,fulana za NMB pamoja na mabegi
ya shule kupitia promosheni ya Jenga maisha yako na NMB.
Katika droo ya kwanza washindi zaidi ya 167 walijishindia zawadi mbalimbali.
Kushinda ni rahisi sana, fungua akaunti au ongeza amana kwenye NMB
Bonus Account au NMB Junior Account upatea riba ya kuvutia ambayo inaweza
kuwa hadi asilimia
10 kutegemeana na kiwango cha amana ilichoweka.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)