Benki ya NMB imeendelea kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa wateja kwa
kuongeza matawi zaidi ya 143 na mashine za ATM zaidi ya 450 nchi nzima.
Katika kuboresha huduma zake, NMB imefungua kituo maalum kwa ajili
ya kuhudumia wafanyabiashara, wateja wakubwa na ofisi za serikali kiitwacho
NMB Mwanza Business Center.
Kwa kupitia kituo hiki, wafanyabiashara na wateja walengwa watapata
huduma kutoka mazingira yaliyo boreshwa zaidi na kwa ufanisi zaidi.
NMB Mwanza Business Center ni ya tatu baada ya kituo kama hicho kufunguliwa
Kariakoo, Dar es Salaam na Arusha katika jengo la Arusha Palace.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bw. Mark Wiessing alisema “Ufunguzi wa kituo hiki ni ishara kuwa NMB imejikita katika utoaji
huduma bora kwa serikali, wateja wadogo, wakati na wakubwa. NMB ina
mpango wa kufungua vituo vingine katika mikoa ya Mbeya na Morogoro”
Vile vile, Benki
ya NMB inatarajia kufungua tawi jipya jijini Mwanza katika kitongoji
cha Buzuruga.
Ufunguzi huo ulifuatiwa na sherehe fupi na wateja wa NMB iliyohudhuriwa
pia na Meya wa Jiji la Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo na Mkuu wa Wilaya
ya Nyamagana Bw. Baraka Konisaga.
Wafanyabiashara wa Mwanza Business Center wakibadilishana
mawazo wakati wa ufunguzi huo
Wafanyakazi wa NMB Mwanza Business Center wakiwa
katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bw.Mark
Wiessing wakati wa ufunguzi huo.








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)