Mobile Ticketing' yaboresha huduma zake - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mobile Ticketing' yaboresha huduma zake

Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi kwa njia ya Mobile Ticketing kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo mikoani,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Juma Mgori.

KAMPUNI ya Mobile Ticketing Tanzania Limited imezidi kuboresha huduma zake kufuatia kurahisisha zaidi upatikanaji wa tiketi za kusafiria kwenye Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine muhimu nchini.
Uboreshaji huo umekuja kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu mkubwa wa huduma hiyo katika jamii ili kuzidi kuwarahisishia hata wale wasiokuwa na simu za mikononi waweze kupata huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Afisa Maendeleo ya Biashara  wa kampuni hiyo, Albert Muchuruza, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuwa na huduma hiyo huku ikiendelea kushirikiana na Vodacom kwaajili ya kuhakikisha huduma hiyo ya tiketi popote inamfikia kila mwananchi hapa nchini.
"Tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha vitu vichache japo huduma hii ya upatikanaji wa tiketi za Usafiri wa Mabasi wa Mabasi kupitia  wakala wa Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine za kulipia ANKARA za maji, umeme, ving'amuzi nk, imeshaanza kutumika hapa nchini lengo likiwa ni kuhakikisha huduma hii inapatikana kwa urahisi zaidi na kumfikia kila mtu.
Aidha, Muchuruza alisisitiza kwamba huduma hiyo ya upatikanaji wa tiketi kwenye selcom pay point imekwishaanza kufanya kazi siku chache zilizopita na kuiomba jamii itambue mchango wa kampuni yake ambao ni kurahisisha na kuweka huduma kama hiyo karibu na jamii kitu ambacho ni uzalendo.
Mbali na hayo, pia Muchuruza alisifu muitikio chanya wa wananchi juu ya utumiaji wa huduma hiyo ya tiketi popote na kusema kuwa tathmini iliyofanywa na kampuni yake inaonyesha kuwa jamii imeanza kutambua na kuelewa umuhimu na matumizi sahihi, hadi sasa muitikio ni mkubwa na wenye kuridhisha kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja tangu huduma hiyo kuzinduliwa mapema mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages