Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi, akimkabidhi vifaa
vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dkt.
Alphoncina Mbinda, wakati wa hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye
Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vyenye thamani ya sh.
milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi
wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi
wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya
Kinondoni, Stanley Mkandawile, (wapili kulia), na katikati ya Makamu na
Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.
Wana-CCM Kata ya Kimara wakishangilia wakati wa hafla hiyo.
Wana-CCM
na wananchi wakisebeneka kucheza muziki wa taarab, kushangilia
makabidhiano ya vifaa hivyo vya huduma na tiba kwa Zahanati yao.
Baadhi ya wanachama wa Jumuia ya Wazazi waliohudhuria sherehe hiyo. Picha
na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)