Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akigonganisha
glasi na Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande
Augustine Nanyaro, wakati wa hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza
anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo
kwa takriban miaka 37. Hafla hiyo ilifanyanyika usiku wa kuamkia leo
katika Bwalo la Maafisa wa Magereza la Ukonga, Dar es salaam.
Maofisa
wa ngazi mbalimbali wa Magereza na taasisi zingine wakipita meza kuu
kumuaga Kamishna Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande
Augustine Nanyaro, katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa magereza
anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia jeshi hilo
kwa takriban miaka 37.
Kamishna
Jenerali wa Magereza anayemaliza muda wake, Afande Augustine Nanyaro,
akijumuika na waalikwa katika hafla ya kumuaga kiongozi huyo wa
magereza anayestaafu rasmi mwishoni mwa mwezi huu baada ya kutumikia
jeshi hilo kwa takriban miaka 37.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)