Mtoto Alhaj.
Mtoto Alhaj akiwa amesimama.
Mtoto Alhaj akiwa anatembea.
Abdulatifu Sadik (5) akipata kifungua kinywa nje ya nyumbani kwao.
Mwanaharusi
Juma akiwa nje ya nyumba yake pamoja na watoto wake Ahaj (10) mwenye
shati Nyekundu na Abdulatifu.Picha zote na Nathaniel Limu
---
Mjumbe
wa kamati ya shule ya msingi Ndulungu tarafa ya Ndago wilayani Iramba
mkoa wa Singida, Sadik Suleman Mnyawi (44), amemtelekeza mke wake mdogo
Mwanaharusi Juma (34), kwa zaidi ya miaka miwili na kumsababishia maisha
kuwa magumu.Imedaiwa kwamba Mnyawi amemtelekeza mke wake huyo, kwa madai kwamba amezaa watoto wawili wanaofafana na nyani.
Mjumbe
huyo wa kamati ya shule, amemtelekeza mke wake mdogo na kumpora nguo
zote na kumwachia zile alizokuwa amevaa tu. Pia aliondoka na matandiko
yote ya kitandani na kubakisha chaga pekee.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwanaharusi awali alikuwa ameolewa na mwanaume
mwingine waliobahatika kupata mtoto mmoja, Fadhili Juma (15).Alisema
baada ya kuachana na mwanaume wa kwanza, mwaka 2002, aliolewa na Mnyawi
ambaye amemtoroka na kumwacha bila matunzo yoyote ya watoto watatu
aliozaa naye.Alisema
katika kipindi cha miaka 10 ya ndoa yake na Mnyawi, walifanikiwa kupata
watoto watatu kati yao, wawili wakiwa wanafanana na nyani.
“Mtoto
wangu yule niliyezaa na mume wa kwanza, Fadhila Juma, yeye yupo darasa
la saba mwaka huu. Ramadhani (6) ambaye nimezaa na Mnyawi, yeye
anasoma darasa la kwanza hapa Ndulungu”,alisema.
Mwanaharusi
alisema kwa watoto wake aliozaa na Mnaywi,Alhaj (10) na Abdulatifu (5)
ambao wana sura ya mnyama kutokana na hali zao zilivyo, wameshindwa
kuanza shule.
Akifafanua zaidi, alisema watoto hao wanaofanana na nyani, hawasikii wala hawasemi. Mawasiliano yao yanategemea ishara tu.
“Ukiacha
matatizo yao ya kutokusikia na kuzungumza, pia wanahema kwa tabu
kubwa. Kama huwaoni, ukisikia wanavyohema, unaweza ukafikiria kwamba
hao zio binadamu ni nguruwe anahema”,alisema kwa masikitiko.
Mwanaharusi
alisema mikono yao ni midogo mno na mifupi na ni dhaifu, matumbo na
macho yao ni makubwa. Alhaji pekee ndiye mwenye uwezo wa kusimama na
kutembea umbali mfupi na mwenendo wake unafanana na wa nyani.
Hata
hivyo, alisema watoto hao wawili aliwazaa wakiwa wana sura za binadamu
na afya zao zikiwa njema kabisa. Lakini wakati wanaendelea kukua, ndipo
walipoanza kuugua mara kwa mara na kisha kubadilika sura.
“Wakati
bado tunaelewana na mume wangu, tuliwahi kumpeleka Alhaji katika
hospitali ya mkoa wa Singida. Alichunguzwa na alibainika kuwa na
upungufu wa damu. Aliongezewa damu na kisha tuliruhusiwa kurudi
nyumbani”,alisema.
Alisema
baada ya kurudi nyumbani, haikuchukua muda, Alhaji alianza kuugua tena
na baada ya kumshawishi mume wake Mnyawi, wampeleke hospitali ya rufaa,
ndipo alipomkimbia na kuhamia kwa mke wake mkubwa.
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa,alisema kuanzia wakati huo, anaishi maisha
magumu mno ambayo ni ya kuomba omba. Mnyawi pamoja na familia yake,
amewabembeleza wamsaidie mizigo wa kuwalea watoto hao, wamegoma kabisa.Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho, Idd Nyauli, alisema
wamejitahidi kumshauri Mnyawi amrudie mke wake mdogo ili waweze kuwalea
watoto wao pamaja, jitahida hizo zimegonga mwamba baada ya Mnyawi
kugoma kumrudia Mwanaharusi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)