Mkurugenzi wa masoko wa
kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia akikabidhi
zawadi ya jenereta kwa mshindi wa promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo
inayoendeshwa na kampuni hiyo hapa nchini, pamoja naye ni wafanyakazi wa
kampuni hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro.
Zawadi hizi zilikabidhiwa jana
kwa washindi waliopatikana katika kitongoji cha kiboroloni na majengo mkoani Kilimanjaro.
Picha ya pili ni Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda
mkoani humo wakimpongeza bodaboda mwenzao Bw. Rogers kavishe abaye
amejishindia jenereta sambamba na Bw. Vicent Lymo ambaye naye
amejishindia jenereta.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru
akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi ya
jenereta kwa mshindi.
Bw. Deusdedit Tobias Njau 22akifurahia na wenzake mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Jenereta.
Kampuni ya bia ya Serengeti jana
imekabidhi zawadi ya jenereta mbili kwa washindi wa zawadi hizo katika
kitongoji cha kiboroloni moshi mkoani Kilimanjaro ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16za promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni
washindi wawili walipatikana ambao ni Bw. Deusdedit Tobias Njau 22
kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya
na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano
hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa
vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa
na umati mkubwa wa watu
ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na
kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo
ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa
nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru amesema washindi hao walipatikana
kihalali na kwamba kila mtanzania mweneye sifa zilizoainishwa katika
vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na
kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika
promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini siku chache
zijazo tutakuwa hapa tena kwaajili ya kumkabidhi mshindi mwingine
pikipiki mpya” alisema Mafuru na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi
mema na kampuni ya bia ya Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya
mtu haiwezi kwenda kwa mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita mfululizo ambapo bado takriban wiki 16
sasa ili kuisha kwa promosheni hiyo ya pekee na aya kwanza kutokea hapa
nchini ambapo zaidi ya milioni 780 za kitanzania zinashindaniwa kote
nchini
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)