Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza Kusitisha Kutoa Tamko La Serikali Kuhusu Mgomo wa Madaktari Nchini - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza Kusitisha Kutoa Tamko La Serikali Kuhusu Mgomo wa Madaktari Nchini

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda
---
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake  kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo.

Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharula, kwa kuwaita madaktari wasitaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali, kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma.

Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.

Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dk. Ulimboka ametekwa na kupigwa alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.

Alisema kuwa amemuagiza, Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages