Mratibu
wa Shindano la Miss Dar Intercollege 2012, Dina Ismail akiwanadi
warembo watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege 2012 wakati wa
uzinduzi wa bendi ya SkyLight ndani ya Mafian Lounge jijini Dar es
Salaam wikendi iliyopita.
Wakipita wa mwendo wa twiga...
Wakifunguliwa shampeni kwa nderemo na vifijo.
Baadhi
ya Warembo wa Miss Dar InterCollege wakiwamejipanga mbele ya wadau na
wadhamini katika uzinduzi wa bendi ya SkyLight iliyofanyika Mafian
Lounge iliyopo Masaki, bendi hiyo inamilikiwa na mmoja wa wadhamini wao
Ndege Insurance.
Mratibu
wa Shindano hilo Dina Ismail alisema kwamba warembo watakaoshiriki
shindano hilo wanaendeleza na mazoezi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar
es Salaam chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa
shoo wakinolewa na Bob Rich.
Alisema
mpaka sasa warembo 15 kutoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa
Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii na kile cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) wamesharipoti kambini.Dina
aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Hilda Edward, Nancy Maganga,
Saada Seleman, Neema Nashon, Rose Muchunguzi, Fina Revocatus, Jane
Augustino,Theresia Issaya na Natasha Deo.Taji la kitongoji hicho
linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM.
Kwa
upande mwingine, mratibu huyo ameyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza
kudhamini shindano hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake na hasa
ikizingatiwa kuwa washiriki wake wana vigezo vya hali ya juu.
“Tunaomba
makampuni mbalimbali yajitokeze kudhamini shindano letu…mpaka sasa
wadhamini tulionao ni pamoja na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia
bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege Insurance, Dodoma Wine na Clouds Fm.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)