Na Mwandishi Wetu
WAREMBO
wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano
ya keshjo wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club
Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano
hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho
ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo
msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.
Mratibu
wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata
kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta'
kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.
Dina
alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza
kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la
kujipoza baada ya mazoezi yao.
"Warembo
wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta
hutumbhuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaoomba
mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa
katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,". alisema
Alisema
maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14
watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa
iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
“Mwaka
huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar
Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema
Dina.
Warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE),
Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha
(IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya
kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga
fainali za Miss Tanzania.
Dina
aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose
Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema
Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha
Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano
hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen
Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada
Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi,
Sufianimafoto, Dinaismail(zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa
na Fullshangwe.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)