Mratibu
wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji
miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI)
unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba
wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye
lengo la kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika
mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22
nchini Brazil kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye
pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise Chamberlain. Kulia
ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
Mratibu
wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji
miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI)
unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akielezea
Utekelezaji wa MKUHUMI ambao umejikita katika kupunguza hewa ukaa kwa
kutekeleza shughuli kama vile Kuzuia ukataji miti ovyo
(Deforestation), Kuzuia uharibifu wa misitu (Forest
Degradation), Uhifadhi wa Misitu (Forest Conservation), Usimamizi
endelevu wa misitu (Sustainable Forest Management) na Kuongeza uwezo wa
misitu kuhifadhi kaboni (Enhancement of Carbon Stock).
Bw.
Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo
endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika
mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo
sasa".
Bw.
Muyungi ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua
zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo
endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata kanuni za usawa huku
tukitambua tofauti katika uwajibikaji na uwezo.
Upatikanaji
wa njia mpya, za ziada, thabiti, zinazotabirika za kupata fedha kwa
ajili ya kutekeleza shughuli za usimamizi wa mazingira na maendeleo
endelevu kwa nchi zinazoendelea.
Mtaalamu
wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu
umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale
inapotaka kwenda. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa
Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala
ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo.
Mmoja
wa Washiriki akichangia maoni yake kuhusiana na nini kifanyike ili
waandishi wa habari waweze kuwa na ufahamu na elimu ya mazingira na
kuizungumzia kwa jamii.
Bi.Gertrude
Lyatuu (kulia) kutoka Umoja wa Mataifa akizungumzia mfumo wa
uwezeshaji utakaopelekea uzalisha, usambazaji na matumizi ya bidhaa na
huduma ikiwa ni matokeo ya kuboresha maisha ya mwanadamu kwa muda mrefu
kwa kutunza mazingira bila kukiangamiza kizazi kijacho.
Afisa
Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo
akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard
Muyungi (hayupo pichani).
Baadhi
ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini walioshiriki warsha
iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mtaifa kuhusiana na Umuhimu wa
kufahamu na kutunza mazingira ikiwa ni katika Siku ya kuadhimisha
Mazingira Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Washiriki
kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakiwa katika warsha
inayohusiana na mkutano wa Rio+20 iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa
katika kusheherekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)