Afisa
Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akipokea Tuzo
ya utoaji bora wa huduma ijulikanayo kama ‘Century International Gold
Quality ERA Award’, kutoka kwa Rais na Afisa mtendaji mkuu wa taasisi ya
Kimataifa ya Business Initiative Directions, Jose Priento mjini
Geneva-Uswisi. Twiga Bancorp imepata tuzo hiyo,kwa utoaji huduma
zinazoridhisha kwa wateja, Uongozi bora, Mipango mkakati inayokidhi haja
ya wateja kama inavyotambulika katika QC 100 TQM.
Hivi
karibuni Benki hiyo ilitunukiwa Tuzo ya Dhahabu iliyotolewa na jijini
Geneva Uswis, tuzo hiyo inajulikana kama Century International Gold
Award (ERA).
Lengo
la tuzo hiyo ni kutambua ubora wa huduma zitolewazo kwa wananchi na
taassisi au kampuni mbalimbali lengo lokiwa ni kuhamasisha utolewaji wa
huduma bora kwa wateja.
Mtendaji
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo amesema kwamba Benki yake
ilikuwa miongoni mwa Benki 100 zilizoshinda katika tuzo hizo kutoka
nchi 47, tuzo hizo ziligawanywa katika makundi saba.
Amesema kujituma miongoni mwa wafanyakazi katika kuwahudumia wateja pamoja na ubunifu ndio siri kubwa ya mafanikio.
Twiga Bancorp ni Benki inayo milikiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja (100%).
Afisa Mtendaji wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akiwa na baadhi ya maofisa wa BID mjini geneva kabla ya kuanza utoaji Tuzo.
CEO wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo akisalimiana na Rais na CEO wa BID, Jose Priento mjini Geneva-Uswisi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)