Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCR), Fredrick Ntobi.
Waanzania
wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya anaelojia
kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu
matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Frederick Ntobi amesema kuwa kuanzia Januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.
Amesema kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013 dunia nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika luninga zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.
Amengeza kusema ku wa ili mfumo huoi ukamilike ni vema jamii ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa katika ubadilishaji huo.
Bw Ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia bili ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye luininga zao.
Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni nmengi ya utangazaji.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)