Mfanyakazi wa TBL, akimvisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kifaa cha kuzuia vumbi kabla ya kuanza kufanya usafi.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mushi (kushoto) na Steve Kilindo wa TBL wakifagia
ikiwa ni ishara ya kuzindua rfasmi maadhimisho hayo karibu na Soko la
Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiungana na
watumishi wa Manispaa ya Ilala kufanya usafi wa mazingira katika
makutano Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Muheza, Karikaoo, Dar es Salaam
jana. TBL ilitoa msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil. 12
kwa Manispaa ya Ilala wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya
Mazingira, Dar es Salaam jana.
Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Oriyo (katikati), akizoa taka wakati wa kampeni hiyo ya usafi wa mazingira
Watumishi wa Manispaa ya Ilala na Wafanyakazi wa TBL, wakifanya usafi kwenye Mtaa wa Muheza, Kariakoo.
Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo
(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, msaada wa
vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 12 kwa ajili ya Manispaa
ya Ilala, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, Dar es
Salaam jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, akiendesha moja kati ya matolori
yaliyotolewa msaada na TBL kwa Manispaa ya Ilala. Kulia ni Steve
Kilindo wa TBL.
Mtaa wa Muheza, Kariakoo ukipendeza baada ya kufanyiwa usafi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)