Taswira Mbalimbali Za Muendelezo Wa Operesheni Okoa Kusini inayofanywa na CHADEMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Mbalimbali Za Muendelezo Wa Operesheni Okoa Kusini inayofanywa na CHADEMA

 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akihutubia maelfu ya wananchi Masasi mjini
Mbunge wa jimbo la Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akipandisha bendera ya chama nje ya ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula
  Pichani ni Mwenyekiti Freeman Mbowe akikata utepe wa kufungua Ofisi ya CHADEMA Kijiji cha Mkangaula. Ilikuwa ni baada ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoa hotuba ya ufunguzi na John Mnyika kupandisha bendera ya chama nje ya ofisi hiyo, ikiwa ni ishara ya kupiga hatua katika mapambano ya awamu ya pili.
 Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika akitoa 'somo' kwa wanakijiji wa vijiji vya Kata ya Lumesule. Mapema Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika alikaribishwa na kuzungumza na Katibu wa Tawi wa CUF, Bi. Zaituni. Wananchi walimwelewa vyema. Kadi zikauzwa vizuri. Akaacha uongozi wa muda wa tawi lenye wanachama wa 34. Katika Kijiji hicho cha Lumesule,
  Mwananchi mmoja kwa jina la Yasin Mohamed alihoji Ya Mbunge wa Ubungo(CHADEMA)John Mnyika (Kulia)ilikuwaje CHADEMA wakaachia Dkt. Slaa ashindwe urais, wakati alichaguliwa kwa kura nyingi na wananchi na wao wanajua alishinda uchaguzi huo wa mwaka 2010.

 John Mnyika akiwa katika vijiji vya Kata za Makukwe na Mkwedu, wilayani Newala. Kwa George Mkuchika ambako alikutana na kiashiria cha wazi kuhusu udhaifu wa Waziri Mkuchika (Mbunge wa Newala) katika kusimamia majukumu yake, baada ya wananchi katika Kijiji cha Tengulengu, Kata ya Mkwedu kumlalamikia kuwa Diwani wa Kata hiyo, Juma Dadi hajawahi kufungua ofisi yake zaidi ya mwaka mmoja sasa. Pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa barua Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala na kwa Mbunge wao, Mkuchika, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
 Unaweza kuona pia wanawake wakiitikia PEOPLES POWER, nao wakaipiga ya nguvu kweli kweli kuonesha umoja na mshikamano katika Falsafa ya Nguvu ya Umma ya CHADEMA, katika kudai uwajibikaji, kupigania haki, uhuru na mabadiliko ya kweli ya mfumo na utawala nchini.
 
 Sehemu ya Umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Slaa akizongwa na wananchi wa Kijiji cha Namahinga, Masasi aliokuwa akisalimiana nao.
 Opresheni Okoa Kusini katika picha, hapa ilikuwa Masasi Mjini. Waweza kuona katika baadhi ya picha watu walivyopanga mstari kupigania kadi.Picha na Habari na Kurugenzi ya Habari- CHADEMA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages