Meneja
wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redds Miss
World Tanzania 2012 litakalofanyika jijini Dar Es Saam katika ukumbi wa
324 Club uliopo Mikocheni jumamosi 16/06/2012,Kushoto ni Mkuu wa
Itifaki wa Kamti ya Miss Tanzania, Oscar Makoye na Katikati ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa
mashindano ya urembo hapa nchini, Hashim Lundenga. Kampuni ya Bia
Tanzania kupitia kinywaji cha Redds ndio wadhamini wakuu wa Miss
Tanzania.
********
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo
imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha
taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana
kama “Miss Wold 2012.
Akizungumzia
Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012”
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa
mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua
wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii
inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka
mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa
yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya
mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na
kumalizika Septemba.
Ili
tusipoteze nafasi yetu ya kushiriki mwaka huu, kamati ya Miss Tanzania
kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano dogo “Mini competition”
ambalo litatupatia mshindi atakae wakilisha Taifa katika mshindano hayo
makubwa Duniani.
Warembo 10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June katika ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni.
Mshindi
atazawadiwa pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi
yote kwa ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya
Miss World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China.
Kutokana
na umuhimu wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss
Tanzania, kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu,
nao bila kusita wakakubali. Hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango
wao mkubwa katika tasnia ya Urembo hapa nchini.
Akizungumzia
maandalizi ya shindano hilo, meneja wa kinywaji cha Redds, Bi. Victoria
Kimaro alisema; kwa upande wetu Redds, maandalizi yote yapo tayari,
tunatarajia kuwa na shindano lenye mvuto wa aina yake, na litakuwa ndani
ya ukumbi mpya wa kimataifa wa 327 kama mlivyosikia. Shindano hili
litaanza saa Mbili usiku hadi saa Nne na litakuwa kwa waalikwa tu.
Tumeandaa burudani za kutosha na tuna uhakika waalikwa watakaokuja kushuhudia mchakato huu wataridhika na maandalizi haya.
Mabadiliko
haya ya ratiba za Miss World yataathiri ratiba zetu kwa mwaka huu tu,
lakini yatakuwa na matunda mazuri kwetu kwa siku za usoni, kwani Redds
Miss Tanzania atakaeshinda mwaka huu atapata muda mwingi na wa kutosha
kujiandaa kwa ajili ya mchakato wa mashindano yajayo ya Miss World.
Tuna
imani kubwa kuwa wadau wa tasnia ya Urembo wataonesha ushirikiano wao
katika kufanikisha shindano hili na yote yajayo, ili kuinua tasnia ya
Urembo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)