Balozi wa Ghana Mhe.Kingsley Saka Karimu akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Eritrea akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Israel mhe. Gil Haskel akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Ghana Mhe.Kingsley Saka Karimu akiwasilisha hati za utambulisho
Balozi wa Ukraine Volodymyr Butiaha akiwasilisha hati za Utambulisho
Mhe.Raymond Tschibanda akiwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Joseph kabila
Mhe.Nhial Deng Nhial akiwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Salva Kiir.Picha na Freddy Maro -IKULU
---
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea hati za mabalozi
watano wanaoziwakilisha nchi zao hapa pamoja na kupokea wajumbe wawili maalum
waliotumwa na marais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Rais Joseph Kabila wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Mabalozi waliowasilisha hati za utambulisho
ikulu ni pamoja na Mhe.Domingo Lucenario wa Phillippines, Mhe.Volodymyr Butiaha
wa Ukraine,Mhe.Beyene Russom Habtai wa Eritrea, Mhe.Kingsley Saka Karimu wa
Ghana pamoja na Mhe.Gil Haskel wa Israel.
Wajumbe walioleta salamu maalum kutoka kwa marais wao ni
pamoja namhe.Raymond Tschibanda ambaye ni Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa DRC
na Mhe.Nhial Deng Nhial ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Sudan ya
Kusini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)