NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA AFRO-RUHR FESTIVAL UJERUMANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA AFRO-RUHR FESTIVAL UJERUMANI

*FFU  Ngoma Africa Band jino kwa jino na washabiki ndani AFRO-Ruhr Festival ! Mjini Dortmund, Ujerumani jumamosi 30 Juni 2012
 Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake kule Ujerumani, wanatarajia  kutingisha jukwaa la Afro-Ruhr Festival, siku ya jumamosi juni 30 mwaka huu, mjini Dortmund,Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja,  aka kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa la aina yake, kwa mashabiki wa muziki katika onyesho hilo ambalo wanakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band aka FFU, bendi hiyo. 

Kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Supu ya Mawe" "Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo ipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" pia zinasikika katika kambi yao FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages