MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA KUKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI UKUMBI WA KARIMJEE JUMANNE SAA 3:00 ASUBUHI - 7:00 MCHANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA KUKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI UKUMBI WA KARIMJEE JUMANNE SAA 3:00 ASUBUHI - 7:00 MCHANA

 Jaji Joseph Sinde Warioba
----
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba kesho, Jumanne, Juni 19, 2012 atakutana na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi - 7:00 mchana kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, na Wajumbe wake waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 6 Aprili na aliwaapisha tarehe 13 Aprili mwaka huu. Tume ilianza kazi rasmi tarehe 1 Mei, 2012.

Katika mikutano hiyo, Mwenyekiti wa Tume atafafanua kazi za Tume, kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 na namna Tume
inavyozitekeleza.Mkutano wa aina hiyo pia utafanyika mjini Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani keshokutwa Jumatano, Juni 20, 2012, kuanzia saa 3:00 asubuhi kwa Wahariri waliopo Zanzibar. Pamoja na Mwenyekiti wa Tume, katika mikutano hiyo ya wazi kwa Waandishi wa Habari pia watakuwepo Wajumbe wengine wa Tume.
   
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
Ohio Street,
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (00 757 500800
--

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages