Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal
--
Na Happiness Katabazi, Brazil
MAKAMU wa rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dk.Mohamed Grarib Bilal leo mchana yeye pamoja na msafara wake uliwasili
salama jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil tayari kwaajili kwaajili ya
kuungana na viongozi wa matiafa mengine ulimwengu kuudhulia mkutano wa
mazingira duniani unaotambulika kwa jina la Rio+20.
Dk.Bilal ambaye amefuatana Waziri wa ofisi yake anashughulikia
mazingira, Tereva Uvisa,Mshauri wa rais Jakaya Kikwete mwandamizi katika
masuala ya kidiplomasia, Balozi Liberata Mulamula na maofisa wengine
waandamizi wa serikali walipokelewa jana na wenyeji wao ambao ni ubalozi
wa Tanzania nchini hapa na serikali ya Brazil.
Tayari wakuu wa nchi mbalimbali wameishawasili jijini Rio de
Jeneiro kwaajili ya kuudhulia mkutano huo wa kihistoaria mbao utaanza
rasmi Juni 20-22 mwaka huu.Miongoni mwa ajenda kuu itakayo jadaliwa ni
uharibu wa mazingira hususani wa ukataji ovyo wa misitu ambao mwisho wa
siku karibu nchi nyingi hivi sasa zimejikuta zikikabiliwa na matito
yatabia ya nchi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)