MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri ujenzi Dkt Jojn Pombe Magufuli(kushoto)(leo) wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea mjini Dodoma.
Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu , Tawala za mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI)  Aggrey Mwanri  akijibu maswali mbalimbali yaliulizwa na Wabunge katika kipindi cha maswali na majibu  (leo) mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA na Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akimuuliza Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda maswali ya papo kwa papo  (leo) mjini Dodoma katika kikao cha tatu cha mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano unaoendelea mjini Dodoma.
Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu ) Stephen Wasira  akiwasilisha Bungeni   (leo) mjini Dodoma taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim  Lipumba  akisikiliza kwa makini taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2011 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliwasilishwa jana (leo)  Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais   (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira.PICHA NA VICENT TIGANYA WA MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages