MASHINDANO
ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika June 15 katika
ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam akizungumza na waandishi
wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super D'
alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki michuano hiyo yenye lengo
la kupanga viwango vya mabondia.Aliwataja baadhi ya mabondia
watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class atakaezichapa na Twalibu,
Mussa Sunga atazidunda na Ally Muhulo,Charo Issa na Shabani
Kaoneka,Dickson Tembo na Raymon Mbwango na Yakubu Abdallahman, Hassan
Mijugu ataoneshana kazi
na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus.
Pamoja
na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofauti vijana
wengi wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau
wa mchezo wa masumbwi kufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na
Kinyogoli Foundation kwa ajili ya kuwapanga katika viwango mbalimbali vya
ubora wa wachezaji, Alitaja baadhi ya mahitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji
wakati wakiwa ulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa
mbalimbali yatakayotumika kwa ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya
kwanza alisema Super D.
Kwa
yoyote mwenye nia ya kusaidia mashindano hayo kwa namna moja au nyingine
anaweza kuwasiliana na kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu
0655928298 au unaweza fika katika klabu ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar
es Salaam vilevile waweza kuwasiliana na kocha Super D
0713/0787-406938 au unaweza fika Klabu ya Ashanti Iliyopo Ilala Soko la Mitumba kwa mawasiliano zaidi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)