Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ni mkurugenzi na
muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai akizungumza na waandishi wa habari
Baadhi ya Vimwana Vilivyoingia kambini
--
Warembo
wa miss universe Tanzania 2012 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye
hadhi ya kipekee Urban Rose Hotel.Hii ni kwaajili ya kujiandaa na
fainali ya Miss Universe Tanzania 2012 itakayofanyika tarehe 29 mwezi
huu wa juni.
Miss
Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa
warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake.Mafunzo hayo
yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika nyanja tofauti
ikiwemo TGNP.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ni mkurugenzi na
muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai
amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mbali na kuongeza semina zaidi
ili kuwasaidia warembo lakini pia imefanikiwa kuongeza mikoa ambapo
mwaka huu wameshiriki warembo kutoka mikoa saba ya Tanzania.
Mbali
na kutafuta warembo tu bali Miss Universe ni kama chuo cha kufundisha
warembo juu ya kujitambua kama mwanamke na kumpa mbinu mbalimbali za
kimaisha.Vilevile mbali na mshindi kupata nafasi ya kutembea nchi
mbalimbali za kimataifa pia hutoa fursa kwa mshindi kupata nafasi ya
kwenda kusoma nje ya nchi kama vile Marekani kwa kupitia mdhamini wetu
mkuu New York Film Academy’’
Kambi
ya Miss universe Tanzania 2012 imekamilishwa na warembo 20 kutoka mikoa
saba ya Tanzania ambayo ni
Dodoma,Arusha,Mwanza,Kilimanjaro,Manyara,Mtwara na Dar es Salaam.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake
wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa
taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa
kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa
na Amanda Ole sululu,2009 Illuminata James,2010 Hellen Dausen na Nelly
Kamwelu ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Le Grande Casino,The
citizen,Urban Rose Hotel,Amina Designs,Dodoma Hotel na New York Film
Academy
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)