Kuanzia
leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile
ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk
Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake
ni mwanadada Mboni Mashimba.
The
Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili
Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7
Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi
ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia
kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha
televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini
Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na
tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika
stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na
mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;
BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?
MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?
BC:
Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo
haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana
gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?
MM:
Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya
Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya
hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana
kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua
kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani
kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa
mama yangu… Ha ha ha haaaaa
BC:
Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu
fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu
wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka
utotoni au la?
MM:
Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda
kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia
nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk
Show haikuwa ndoto yangu hapo awali.Lakini kama unavyojua,maisha huenda
yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu.
Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto
inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi
dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.
BC:
Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania.
Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha
umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini
chanzo?
MM:
Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la
ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na
hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio
sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa
watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa
wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na
uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na
watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha
ha haaaa
BC:
Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The
Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The
Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?
MM:
Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu
mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka
minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na
rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja
muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala
hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe
hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika
most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia
hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio
hapa tulipo hivi sasa
Read more: UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA - BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)