Mkurugenzi
Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno
wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE
MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na
manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi
ya jinsia ya kike katika jamii.
Mmoja
wa washiriki wa uzinduzi huo Bi. Chansa Kapaya akitoa neno la shukrani
wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za
wanawake wanaokutwa na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania.
Mtunzi
wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo
akielezea simulizi ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji
wa Kijinsia wakati wa usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa
kuweka uzoefu huo katika maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya
unyanyasaji wa Kijinsia unaokua kwa kasi nchini Tanzania.
Mgeni
rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho akitoa nasaha
zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam. Alisema
66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na
majanga ya unyanyasaji wa Kijinsia katika maelzi yao ambapo kwa sasa
Dar es Salaam na Mbeya zinaongoza.
Mgeni
rasmi Dkt. Mrisho na Mtunzi wakionyesha Kitabu kwa wageni waalikwa na
waandishi wa habari. Kitabu hiki kinapatikana katika Maduka ya MKUKI NA
NYOTA PUBLISHERS yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa gharama ya
shilingi 10,000/=.
Jopo la Wataalam wa Mambo ya Jinsia Tiba na Vitabu wakiwa kwenye picha pamoja.
Mkurugenzi wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Mzee Bugoya akibadilishana mawazo na Dkt. Mrisho pamoja na Bi. Kapaya wakati wa uzinduzi
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo baada ya uzinduzi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)