Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame Makundi
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo hii katika makao makuu
ya Tigo Jijini Dar es Salaam juu ya uzinduzi wa huduma mpya ya tigo
inayokwenda kwa jina la 'TIGO INTERNET MEGA BOKSI' ambapo alisema kuwa
wateja wa tigo wataweza kujipatia vifurushi vipya vya mtandao vinavyo
endana na mahitaji yao. Makundi alisema kuwa Mteja wa Tigo ataweza
kununua kifurushi cha siku, wiki, au mwezi pamoja na kufanya uchaguzi
unaoendana na matumizi mbali mbali ya huduma za kimtandao.alielezea
namna ya kupata vifurushi hivyo kuwa ni, kwa kupiga *148*01# ambapo
wateja watapata fursa ya kuchagua muda wa viofurushi wanavyovihitaji
kulia ni Alice Maro afisa habari wa Tigo..
Alice Maro afisa habari wa Tigo akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari alipoulizwa kuhusiana na huduma hiyo mya.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakifuatilia uzinduzi wa huduma hiyo.
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa
yakitolewa na Meneja wa Operesheni za huduma za Internet Tigo Bw, Kwame
Makundi.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)