FFU WA NGOMA AFRICA KUWASHA MOTO NDANI YA AFRO-RUHR FESTIVAL MJINI DORTMUND, UJERUMANI JUMAMOSI JUNI 30. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

FFU WA NGOMA AFRICA KUWASHA MOTO NDANI YA AFRO-RUHR FESTIVAL MJINI DORTMUND, UJERUMANI JUMAMOSI JUNI 30.

 JINAMIZI LA MUZIKI KUSUMBUA TENA ULAYA, Wanamuziki wa kundi la FFU Ngoma Africa, wakiwa jukwaani katika moja ya maonyesho yao.

Sehemu ya mashabiki wa bendi ya FFU, wakifurahia burudani kutoka kwa bendi hiyo.
***********************************
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea jukwaa la Afro-Ruhr Festival, siku ya jumamosi 30 Juni 2012 mjini Dortmund,Ujerumani kuwasha moto.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa na mwanamuziki, Ebrahim Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa na la aina yake kwa mashabiki wa muziki katika onyesho hilo, ambapo  watakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.

Bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Supu ya Mawe" ,''Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo zipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" pia zinasikika katika kambi yao FFU
at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages