Bongo Star Search kuanza ziara ya Kusaka vipaji mkoani Dodoma June 15 - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Bongo Star Search kuanza ziara ya Kusaka vipaji mkoani Dodoma June 15

Na Mwandishi Wetu

ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.

Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.

Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.

“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages