Bia ya Kibo Gold yazinduliwa kwa kishindo mjini Moshi,wanywaji wafurahi kinywaji chao murua kabisa kimerudi. - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Bia ya Kibo Gold yazinduliwa kwa kishindo mjini Moshi,wanywaji wafurahi kinywaji chao murua kabisa kimerudi.


Meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti,Allan Chonjo akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa utambulisho mpya wa kinywaji cha Kibo Gold.Akizungumza na wageni waalikwa na waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika katika kiwanda cha Serengeti tawi la moshi mkoani Kilimanjaro, Bw.Allan Chonjo amesema kuwa kampuni yao imeamua kukizalisha kinywaji hicho na kukirejesha tena kwa wanywaji wake ambao walikikosa kwa muda wa miaka kumi tangu kilipoachwa kuzalishwa.
Meneja wa Kampuni ya Sbl,tawi la Moshi,Bw.Gerald Mandala akitoa historia fupi kuhusiana na na kinywaji cha Kibo Gold,kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wanahabari (hawapo pichani),wakati wa utambulisho mpya wa kinywaji hicho uliofanyika kwenye viunga vya kiwanda hicho cha SBL Moshi.kuliwa kwake ni Operesheni Meneja wa Kiwanda,Bi.Alice Kilembe.
Kinywaji cha Kibo Gold kilichopotea kwa wanywaji wake takribani miaka kumi,kimerejeshwa tena kampuni ya bia ya Serengeti.
Mpishi wa bia ya Kibo Gold,Bw.Julius Nyaki akifafanua  jambo kuhusiana na upishi wa kinywaji cha Kibo Gold bia.
Baadhi ya wafanyakazi wa SBL wakifurahi jambo kwa pamoja.
Wafanyakazi,wadau mbalimbali wakiwemo na wahahabari wakiw kwenye moja ya ukumbi wa kampuni ya SBL,mjini Moshi jioni ya leo kushuhudia utambulisho mpya wa kinyaji cha Kibo Gold.
Baadhi ya wadau wa kampuni ya Bia ya SBL,wakiwa kwenye utambulishao mpya wa kinywaji cha Kibo Gold,uliofanyika jioni ya leo kwanye viunga vya kampuni hiyo,mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages