Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego akisisitiza jambo wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA.Wengine kulia ni Mhandishi Joel Chacha kutoka malaka ya mawasiliano nchini (Tcra) na Kaimu Mratibu wa Jukwaa hilo Agnes Kimwaga.
Bw. Joel Chacha kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii iliyohusu Teknolojia ya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya Sanaa na Wasanii.Kulia ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego.
Mdau kutoka Mlimani TV akiuliza maswali kuhusu mfumo wa Digitali Mmoja wa Wasanii aliyehudhuria mjadala huo akitoa ya moyoni kuhusu mchakato wa kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda ule wa Digitali na mchango wake kwenye Sanaa.
Sehemu ya wadau wa Sanaa waliohudhuria mjadala huo wakifuatilia kwa makini elimu iliyokuwa inatolewa.
Baraza
la Sanaa laTaifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya
kuhimili ushindani wakimataifa kutokana na ujio wa mfumo wa digitali
ambao utazifanya kazi zaokuonekana kimataifa.
Wito
huo umetolewawiki hii kwenye ukumbi wa BASATA na Katibu Mtendaji wa
baraza hilo, GhoncheMaterego wakati akihitimisha mjadala kwenye Jukwaa
la Sanaa uliohusu Teknolojiaya Digital na Faida Zake Katika Sekta ya
Sanaa uliochokozwa na MhandisiJoel Chacha kutoka mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA).
Alisema kuwa, mfumowa digitali utaruhusu uwepo wa vituo vingi vya redio na runinga ambavyovitakuwa na masafa ya kimataifa hivyo ni wazi wasanii wanatakiwa kujipangakatika kuandaa maudhui bora, ya kutosha na yenye mvuto kwa ajili ya kukidhiongezeko hilo na zaidi ushindani wa kimataifa.
“Wasanii
tujipange,fursa zinazokuja ni nyingi mno, zinahitaji maudhui ya
kutosha, yenye ubora nayatakayoweza kuvifanya vyombo vya habari viweze
kuhimili ushindani pia”alisisitiza Materego.
Aliongeza
kuwa,moja ya eneo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wamiliki wa vyombo
vya habari niuhafifu wa maudhui ya kazi za Sanaa hivyo, wasanii hawana
budi kuachakulalamika na kujipanga kukabili changamoto hiyo.
Awali
akiwasilishamada hiyo,Mhandisi Chacha alisema kuwa, mfumo wa digitali
utazalisha fursanyingi katika sekta ya Sanaa lakini akasisitiza kuwa,
uchangamfu wa Wasaniiwetu ndiyo utawafanya wafaidi.
Alizitaja
baadhi yafursa hizo kuwa ni pamoja na; ongezeko la ajira kwa Wasanii,
ongezeko lavipindi, kukua kwa ushindani katika ubunifu na utengenezaji
maudhui yenyeubora, Sanaa za Tanzania kutangazika kimataifa na
kuongezeka kwa makampuniyatakayojihusisha na sekta ya Sanaa
“Mfumo
wa digitaliuna mazuri mengi lakini kubwa ni kuongezeka ushindani na
ubora katikakutengeneza maudhui yenye ubora na pia ongezeko la masafa
katika televisheniambayo yatahitaji maudhui (vipindi) ya kutosha”
Aliongeza Chacha.
Hata
hivyo,aliitaja changamoto ya uharamia kwenye sekta ya Sanaa ambapo
aliwashaiuriwasanii kuamka na kujiunga na Chama cha hakimiliki (Cosota)
ili kuhakikishakazi zao zinalindwa kisheria.
Wadau
wengiwaliochangia mjadala huo walionekana kuwa na wasiwasi na mfumo wa
digitalilakini wakaomba elimu ya kutosha itolewe ili wananchi wengi
zaidi waelewe ninimaana ya kutoka mfumo wa analogia kwenda ule wa
digitali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)