Naibu
Katibu Mkuu akiwa pamoja na mwenyeji wake na waalikwa wengine
walioshiriki chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi Daniel Bodini
wa San Marino. kutoka kushoto ni Bw. Parfait Onanga Anyanga,
Mkurugenzi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Balozi wa Mongolia, Bi.
Enkhtsetseg Ochir, Balozi wa Nigeria, Bibi. Joy Ogwu, Balozi Bodini,
Dkt. Asha- Rose Migiro na Bw. Vijay Nambier aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa
Ofisi ya Katibu Mkuu na ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mwakilishi
Maalum wa Ban Ki Moon huko Myanmar.
---
Balozi
wa Jamhuri ya San Marino katika Umoja wa Mataifa, Bw. Daniele
Bodiniamemuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose
Migiro kama kiongozi ambaye katika uongozi wake daima aliweka mbele
maslahi ya nchi zote bila ya kujali ukubwa au udogo wa nchi.
Balozi
Bodini ametao kauli hiyo siku ya jumatano wakati alipomuandalia
chakula cha mchana Dkt. Asha-Rose Migiro kumshukuru kwa mchango wake na
ushirikiano aliouonyesha wakati wa uongozi wake.
Chakula
hicho cha mchana kiliandaliwa katika makazi ya Balozi Bodini na
kuwashirikisha pia Balozi wa Nigeria katika Umoja wa Mataifa Bibi Joy
Ogwu, na Balozi wa Mongolia Bi. Enkhtsetseg Ochir. Aidha Balozi huyo
wa San Marino Akasema yeye binafsi anashukuru kwa kupata nafasi ya
kufanyakazi kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu katika maeneo mbalimbali
yakiwamo utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia, uanzishwaji
wa UN -Women, masuala ya Ulinzi na Usalama na System wide Coherence.
Vile
vile akasema Migiro amekuwa mfano wa kuigwa na wanawake, wasichana
na watoto wa kike ambao wanamchukulia yeye kama kielelezo cha mafanikio
ya wanawake na kwamba ameatia moyo wengi. Akabainisha kwamba yako
mambo mengi ambayo Migiro ameyafanya wakati wa uongozi wake na kwamba
hapana shaka yataendelea kukumbukwa katika Umoja wa Mataifa.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu akamshukuru kwa heshima hiyo na kwa
ushirikiano aliompatia katika, pamoja na mambo mengine kutekeleza
majukumu aliyokuwa amekabidhiwa ya kumsaidia Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa. Akasema daima ataienzi heshima hiyo na kuwashukuru wale wote
ambao wameshirikiana naye kwa karibu katika utekelezaji wa masuala
mengi na muhimu kwa maendeleo ya mwanadamu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)