Naibu waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala akizungumza na
waandishi wa habari leo hii jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi
bendera kwa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inayokwenda Nchini
Ivory coast kucheza na timu ya taifa ya nchi hiyo jumamosi ya wiki hii
ambapo aliwataka wachezaji wa timu hiyo kuipa raha Tanzania kwa kishindo
kizito na kuwatangazia kuwa wasiogope wachezaji wa Ivory coast
makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tansoma jijini
Dar es Salaam
Rais wa shirikisho la Mpira Tanzania TFF Bw, Leodger Tenga akiwatakia
wachezaji hhao kila la heri katika safari yao na kuwatakia ushindi
mwema.
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Kim Paulsen akiwahakikishia
watanzania kuwa watakwenda kule Ivory Coast kushinda kwani amewafundisha wachezaji
wake namna ya kujiamini wenyewe na pia kuwa na nidhamu mchezoni ili
waweze kupata ushindi.
Wachezaji wa timu ya Taifa waliohudhuria katika Tafrija hiyo ya kukabidhiwa Bendera.
Naibu waziri wa Utamaduni na Michezo Mh, Amos Makala (kushoto)
akimkabidhi bendera ya taifa kapteni wa timu hiyo Mlinda mlango Juma
Kaseja.(PICHA NA PHILEMONI SOLOMON WA FULLSHANGWE)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)