Wakali wa Kili Music Award 2012 walivyoushusha Mlima Kilimanjaro pale Moshi - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Wakali wa Kili Music Award 2012 walivyoushusha Mlima Kilimanjaro pale Moshi


 Hadija Kopa na wasanii wa muziki wa Bongo fleva, Ali Kiba, Omy Dimpoz, Roma Mkatoliki AT, pamoja na wakali wa Ragge Warriors walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Moshi na kudhihirisha uhalali wao wa kutwaa Tuzo mbalimbali za Kili Music 2012. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.

Pichani juuni Mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiimba jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award iliyofanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Roma Mkatoliki akitumbuiza jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Kilimanjaro.


 DJ Choka akisugua vyombo kuendana na Roma Mkatoliki


 Hapa ni usiku ....


 ...ni mchana


 anastua...huyu ni Gwiji Hadija Kopa akifanya vitu vyake jukwaani hapo Ushirika. Mama alifunika mbaya katika show hii


 Wakali wa ragge kutoka kundi la Warriors from East la mjini Arusha wakitumbuiza mashabiki katika tamasha maalum la Washindi wa Kili Music Award 2012 kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza show wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro  jana.


 Hawa nao walikuwa wakitoa mpya ya kujirusha na kuangukia mgongo. Ni vijana wa Suma Lee.


 Suma Lee akifanya vitu vyake jukwaani



 Msanii anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba leo.


 Nai Nai hapa ikiimbwa maana Omy Dimpoz alimshirikisha Ali Kiba


 Wadau wakifuatilia show hiyo


Ali Kiba akienda sawa na vijana wake, hakika Moshi ilikuwa hapatoshi.Picha/Habari Kwa Hisani ya Father Kidevu Blogu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages