Mkuu wa Idara ya mawasiliano na habari Lilian Liundi akifundisho.
Picha juu na chini Waandishi wanaoshiriki mafunzo wakiwa katika majadiliano
--
WAANDISHI wa habari wameaswa kubeba sauti za wananchi walioko
pembezoni katika kudai haki zao hasa wakati wa mchakato wa kukusanya
maoni ya wananchi kwaajili ya kuandaa katiba mpya.
Akizungumza jana Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichoko
chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Dorothy Mbilinyi, amesema
watanzanzia masikini walioko pembezoni wanategemea kupata taarifa na
kutoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
“Wananchi wameamka wameanza kujieleza vyombo vya habari vinatakiwa
kufanya kazi yake kuwa sauti ya wanyonge, viwe mdomo kwa makundi
yaliyowekwa pembezoni, ili kuibua changamoto zilizojificha na kuyafanya
makundi haya kuwa na haki sawa na wengine,” amesema MbilinyiMbilinyi amesema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania vimefanya kazi
kubwa ya kuibua kero za wananchi na ufisadi, ikiwepo kudai uwajibikaji
katika misingi ya demokrasia na haki za biandamu.
Aidha amewataka
waandishi wa habari kufanya kazi kwa bidii mwaka huu kwasababu ni
mwaka wenye changamoto nyingi ambazo zitahitaji weledi, uadilifu,
ukweli na uwazi.” Huu nini mwaka wa kukusanya maoni ya katiba, mwaka wa
kudai uwajibikaji kwa viongozi wasio waadilifu, na ni mwaka wa Sensa ya
idadi ya watu…” amesema Mbilinyi.
Akieleza malengo ya mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza mei 3 hadi
5, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na habari, Lilian Liundi amesema kuwa
mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kujitadhimini upya jinsi
ambavyo wanaandika habari za kijinsia.
Pamoja na kujitadhimini waandishi wa habari watajifunza juu ya hali
ya sasa ya ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi,
kampeni ya haki uchumi, mfumo dume na mfumo uleberali mambo leo.
Pia
watajifunza namna ya kuandika habari za kijinsia na kuchambua maoni
yanayotolewa na wananchi juu ya katiba mpya, kufanya habari za
kiuchunguzi vijijini na kuibua changamoto za wananchi.
Mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni siku chache baada ya TGNP
kukutana na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es alaam wiki
iliyopita.
Habari hii imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)