TGNP YAWANOA WANAHARAKATI TOKA MIKOANI KATIKA MBINU ZA URRAGHBISHI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TGNP YAWANOA WANAHARAKATI TOKA MIKOANI KATIKA MBINU ZA URRAGHBISHI

Mchoraji wa katoon magazeti ya The Guardian Muhidin Msamba, akimsawadia Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Zawadi ya picha ya kuchora wakati wa mafunzo hayo.
 

Leo TGNP imezindua warsha ya  uraghbishi ya wiki moja  kwa wanaharakati kutoka mikoani pamoja na Dar es Salaam, ili  kunoa uwezo wao wa kufanya kazi na   jamii husika kuibua masuala nyeti katika jamii hizo zikiwemo mafanikio na changamoto, kuchambua visababishi vya matatizo au mafanikio hayo kwa kina  na kupanga mikakati ya kushughulikia kero hizo  pamoja na wanajamii . 
 
Warsha hiyo inalenga kuimarisha uelewa wa pamoja  wa mtizamo  ya  kiitikadi  kuhusu  dhana za ukombozi wa  wanawake kimapinduzi na makundi yaliyoko pembezoni  na kuitekeleza  kwa vitendo;  kujenga uelewa  wa pamoja  kuhusu  uraghbishi  na mbinu shirikishi  zinazotumika  katika uraghbishi,  kuongeza uelewa wa kampeni  ya hiaki ya uchumi  katika kudai kazi zenye heshima utu na kipato, uhifadhi wa kumbukumbu, mbinu za mawasiliano  na uwezo wa kuvitumia  katika Ujenzi wa  Vuguvugu la ukombozi wa wanawake kimapinduzi katika ngazi ya kanda.
 
Wawezeshaji wa warsha hiyo ni  Bw. Richard Mabala   Mkurugenzi wa TAMASHA  ambayo ni asasi  ya kiraia iliyobobea  katika kuwawezesha vijana  na jamii kwa ujumle  kutumia mbinu za uraghbishi  kama chachu ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii husika.  Bw. Winston Chuchil Mkurugenzi Msaidizi wa TAMASHA ni mwezeshaji mwenza  ambaye naye pia amebobea katika mbinu za uraghbishi.
 
Washiriki wa Warsha hiyo wametoka katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Arusha, Dodoma, Mwanza , Mbeya, Dar es Salaam na Pwani wakiwakilisha asasi mbalimbali za kiraia ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii za mikoa husika.
 
Baada ya warsha  washiriki wakishirikiana wanajamii  na TGNP wataendesha zoezi la uraghbishi katika mikoa  husika ambapo watatumia mbinu mbali mbali za uraghbishi katika  kuibua  masuala nyeti yanayogusa jamii husika, kuyachambua kwa kina ili kupata kiini cha matatizo au mafanikio, hayo na  kutafuta  mbinu mbali mbali za  kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo, mbinu zitakazotumika, nani atafanya nini kuanzia ngazi binafsi, jamii  na taifa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages