Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa
Canada Bi. Berly Oda walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya
Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la
Kimataifa la Uchumi kwa Afrika
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Mstaafu Bw Koffi Annan walipokutana katika hoteli ya
Sheraton jijini Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la
Kimataifa la Uchumi kwa Afrika
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Bishara la Kimataifa - World Trade Organisation (WTO)- Bw Paschal
Lamy walipokutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sheraton jijini
Addis Ababa ambako wote walihudhuria Kongamano la Kimataifa la Uchumi
kwa Afrika
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Kongamano la
Kimataifa la Uchumi kwa Afrika, akiwa na viongozi wengine wa nchi
mbalimbali waliohudhuria
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Nigeria Mh Goodluck Jonathan
baada ya kuhudhuria dhifa ya kitaifa waliyoandaliwa na mwenyeji wao
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mh Meles Zenawi jijini Addis Ababa Alhamisi
usiku. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Fedha wa Nigeria Bi.Ngozi Okonjo-Iweala ikiwa ni kielele cha Kongamano la Kimataifa la Uchumi kwa Afrika.Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)