SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA AWASILI NCHINI JAPANI KWA ZIARA YA KIKAZI SIKU 6 KWA MWALIKO WA BUNGE LA JAPANI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA AWASILI NCHINI JAPANI KWA ZIARA YA KIKAZI SIKU 6 KWA MWALIKO WA BUNGE LA JAPANI

    Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkabidhi zawadi Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kufanya nae mazungumzo baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani.
 Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta akimuonesha katika ramani Mhe. makinda sehemu kubwa ya Maeneo yalioathirika na mafuriko hayo katika Mji wa natori.
 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika mazungumzo maalumu na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (kushoto) mara baada ya kuwasili katika mji huo kwa lengo la kujionea uharibifu ulitokana na mafuriko ya tsunami yaliotokea machi mwaka jana ambapo zaidi ya watu 911 walipoteza maisha na wengine 53 kutopatikana katika mji huo. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani. 
 Mhe. Spika akiangalia baadhi ya Mabaki ya wahanga wa Mfuriko hayo katika Shule ya awali ya YORIAGE  ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa
 Mhe. Spika akiangalia baadhi ya Mabaki ya wahanga wa Mfuriko hayo katika Shule ya awali ya YORIAGE  ambapo picha na nguo za wanafunzi waliofariki zimehifadhiwa
   Magari yalioharibika na Mafuriko yakiendelea kuondolewa katika eneo hilo
 Baadhi ya mabaki ya Meli zilizosombwa na mafuriko hayo.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta (Kulia) mara baada ya kuweka shada la Maua katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kumbukumbu ya wahanga wa Mafuriko ya Tsunami yaliyoikumba nchi ya Japan Mwezi Machi mwaka jana alipotembelea Mji wa NATORI, Uliopo mkoa wa MIAGA ikiwa ni mojawapo ya miji iliyokumbwa na mafuriko yaliyoikumba Japani Mwaka jana. Mhe. Spika na ujumbe wa wabunge 5 wapo katika ziara nchini Japani kwa mwaliko maalumu wa Bunge la Japani. Kushoto ni Mhe. Tundu Lissu, Mhe. Anne Makinda, Mhe. Rukia Ahmed, Mhe. James Lembeli, Mhe Anne Kilango Malecela, Naibu meya wa Mji wa Natori Mhe. Takamoto Ohta na Mhe. Godfrey Zambi.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Narita Mjini Tokyo kwa ziara ya siku 6 ya  Mwaliko wa Kikazi kutoka Bunge la japani.  Kulia kwake ni balozi wa Tanzania Nchini Tanzania Mhe. Salome Sijaona. Mhe. Spika katika ziara hiyo ameongozana na Ujumbe wa Wabunge 5 kutoka Bunge la Tanzania.Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Pages