RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI KITAIFA MKOANI TANGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA MEI MOSI KITAIFA MKOANI TANGA

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa kashikana mikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mh, Waziri wa Kazi na Ajira Mh Gaudence Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Galawa katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
 Gari la Kiwanda cha Cementi ya Simba, likipita mbele ya Jukwaa kuu, wakati wa maandamano ya magari ya viwanda yalipokuwa yakiingia uwanjani hapo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Umati wa wafanyakazi na wananchi waliojitokeza katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wakiwa uwanjani hapo wakisikiliza Hotuba ya Rais Kikwete.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu kama zawadi kwa  Mfanyakazi bora wa Tanesco Bi Anetha Chengula  katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.Picha zote na IKULU

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages