Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Ijumaa, Mei 4, 2012, amemteua Bibi Saada Mkuya Salum kuwa Mbunge
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo unaanza mara
moja.
Rais
amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Ibara ya 66 (i) (e)
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama
ilivyorekebishwa.
Chini
ya Ibara hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapewa mamlaka
ya kuteua wabunge 10 kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mpaka
sasa, Rais Kikwete ameteua wabunge saba. Novemba mwaka 2010, aliteua
wabunge watatu na jana, Alhamisi, Mei 3, 2012 ameteua wabunge wengine
watatu ambao ni Professa Sospeter Muhongo, Bibi Janet Mbene na Bwana
James Mbatia.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)